Jumamosi 26 Aprili 2025 - 08:21
Wananchi wa Korea Kusini wakusanyika kulaani uwepo ubalozi wa Israel

Wafuasi wa Palestina na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Korea Kusini walikusanyika mbele ya mgahawa mmoja jijini Seoul, mahali ambapo balozi wa Israel alikuwa amefika kwa ajili ya chakula cha jioni, ili kulaani uhalifu wa kivita unaofanywa na utawala wa Kizayuni.

Shirika la Habari la Hawzalikinukuu kituo cha habari cha al-Manar, siku ya Jumatano video moja ilisambaa kwa kasi kubwa katika mitandao ya kijamii.

Video hiyo ilionyesha wakati ambao wanaharakati wa haki za binadamu na wafuasi wa Palestina walikusanyika mbele ya mgahawa aliokuwemo Rafael Harpaz, balozi wa Israel nchini humo, huku wakipaza sauti kwa kauli mbiu kama vile: "Palestina ni huru" "Muuwaji wa halaiki ondoka hapa", mikono yako imejaa damu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha